Kwa mujibu wa gazeti la ar-Rai kikao hicho kiliwajumuisha wataalamu kutoka nchi za Jordan, Bahrain, Imarati, Saudi Arabia, Yemen, Uturuki, Syria, Tunisia, Palestina na Malaysia.
Washiriki wa kikao hicho wamebadilishana uzoefu kuhusiana na takwimu za Kiislamu na fursa za nchi za Kiislamu zikilinganishwa na nchi nyinginezo katika nyanja tofauti za kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Wataalamu hao wametayarisha mapendekezo ambayo yatawasilishwa katika kikao kijacho cha OIC mjini Istanbul Uturuki.
Washiriki wa kikao hicho wamesisitiza juu ya kubadilishana uzoefu wa kitaalamu kuhusiana na takwimu za Kiislamu ili kuweza kuainisha viwango vinavyofaa vya takwimu za Kiislamu duniani. 716925