Taarifa hiyo imesema kuwa jina la Nabii Masih pamoja na la mama yake mtakatifu Maryam (as) yametajwa mara kadhaa katika Qur'ani Tukufu na kuwapongeza Waislamu na Wakristo kwa mnasaba wa kuzaliwa Nabii huyo Mtakatifu.
Sayyid al-Muhri ameelezea matumaini yake kwamba mwaka mpya ujao utakuwa mwaka wa heri, baraka, utulivu na usalama kwa walimwengu wote. Vilevile ameelezea metarajio kuwa ulimwengu hautashuhudia tena vitendo vya ugadi, vita na matatizo ya kijamii.
Al-Muhri ambaye pia ni Mkuu wa Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Ukristo la Kuwait ameendelea kusema kuwa Uislamu ni dini ya urafiki wa dhati, upondo, usamehevu na maisha ya amani ya pamoja na watu wengine na kwamba Waislamu pia husherehekea siku ya kuzaliwa Nabii Isa (as). Amesema ni makundi ya kitaasubi na yenye fikra potofu yanayowakufurisha watu pamoja na viongozi wao waovu tu ndio huwa na huzuni katika siku hii muhimu.
Sayyid Muhammad Baqir al-Muhri amesisitiza kwamba fiqhi ya Ahlul Bait (as) inajuzisha Waislamu kuwapongeza Wakristo kwa mnasaba wa kuzaliwa Nabii Isa (as) na kwamba mafundisho ya Kishia pia yanakataza wafuasi wake kuwafanyia khiana na maudhi majirani wasiokuwa Waislamu. 717385