IQNA

Wanaokosea heshima Qur'ani Tukufu nchini Russia waonywa na Waziri Mkuu

10:46 - December 27, 2010
Habari ID: 2053912
Vladmir Putin, Waziri Mkuu wa Russia amewaonya watu wanaodharau na kukosea heshima Qur'ani Tukufu ambacho ni kitabu kitakatifu cha Waislamu kwamba watapunguziwa misaada ya afya.
Onyo hilo la Putin linafuatia matukio ya kusikitisha yaliyotokea katikati mwa nchi hiyo katika kipindi cha wiki chache zilizopita ambapo watu kadhaa walifanya vitendo vya kukosea heshima kitabu hicho kitakatifu. Putin amesisistiza juu ya umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani watu wa Russia ambao wanafungamana na makundi tofauti ya imani na utamaduni.
Ameashiria hatari ya kuongezeka mielekeo ya utaifa na ubaguzi wa rangi nchini humo na kusema kuwa jamii mbalimbali za nchi hiyo zinapasa kushajiishwa suala la kuishi pamoja kwa amani na sio kuchochewa kujihusisha na vitendo vya ubaguzi wa kimbari na dini. 719038
captcha