Kikao hicho ambacho kinaandaliwa na Jamiatul Mustafa (saw) al-Alamiyya kimepangwa kufanyika tarehe 5 na 6 Machi mwakani. Kwa mujibu wa tovuti ya india.miu.ac, kikao hicho kitafanyika katika makao ya jumuiya hiyo huko New Delhi.
Lengo la kufanyika kikao hicho ni kubainisha misingi ya kimaadili katika Uislamu, kuchunguza vitabu vya pamoja vya kimaadili katika Uislamu na dini za Kihindi, kunyanyua viwango vya thamani za kimaadili katika jamii na hasa katika vyuo vikuu na vituo vya kielimu na kiutafiti na vilevile kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na suala hilo.
Nafasi ya maadili katika Uislamu na dini za kihindi, misingi ya maadili katika dini hizo na kulinganishwa kwa misingi hiyo ni baadhi ya masuala yanayojadiliwa katika kikao hicho.
Walio na hamu ya kushiriki katika kikao hicho wana muda wa hadi tarehe 31 mwezi huu wa Disemba kuwasilisha makala zao katika moja ya lugha za Kiingereza, Kifarsi au Kiurdu kupitia anwani ifuatayo ya ofisi ya Jamiatul Mustafa (saw) al –Alamiyya nchini India: miu.ethics@gmail.com.
Makala bora zitachaguliwa na kamati husika na kisha kuchapishwa katika sura ya kitabu na hatimaye kugawiwa washiriki wa kikao hicho. 719164