Akiashiria hotuba ya dharau na kukosewa heshima iliyotolewa hivi karibuni na baadhi ya watu majahili na wasofahamu vyema Uislamu katika swala ya Ijumaa katika mji wa Subeika katika mji wa Isa nchini Bahrain, Sayyid Mash'al amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuona kwamba mimbari za baadhi ya misikiti zimebadilishwa na kuwa vituo vya kueneza dharau, chuki, fitina na uongo dhidi ya taasisi na wanazuoni wa Kishia. Amesema la kusikitisha zaidi ni kuona kwamba hotuba hizo za dharau zinatolewa na watu wanaofungamana na serikali ya Bahrain na walio na wawakilishi katika bunge la nchi hiyo.
Amesema dharau dhidi ya Ayatullah Sistani ni uchokozi wa wazi dhidi ya nembo kubwa zaidi ya Ushia nchini Iraq na kwamba itaeneza fitina za kimadhehebu na kusababisha madhara makubwa kwa umoja wa kitaifa na vilevile kuishi pamoja kwa amani wananchi wa nchi hiyo. Ametaka wanaohusika na vitendo hivyo waadhibiwe mara moja na vyambo vya sheria. Amesema Ayatullah Sistani ni kilele cha maarifa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba matamshi ya kijahili yanayoenezwa na baadhi ya watu dhidi yake hayatakuwa na athari yoyote kwa itibari yake kwa sababu amekuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha umoja wa Waislamu na ni nguzo muhimu wa amani na utulivu nchini Bahrain.
Mkuu huyo wa Baraza la Maulama wa Bahrain amesema mwishoni mwa taarifa yake kwamba, ulimi unaohubiri fitina na ghasia nchini Bahrain unapasa kukatwa na kwamba mimbari za swala ya Ijumaa pia zinapasa kuzuiwa kuwa sehemu ya kueneza dharau na uongo dhidi ya taasisi na wanazuoni wa kidini.
Tunakumbusha hapa kwamba, Ijumaa iliyopita ya tarehe 24 Disemba, hatibu wa swala ya Ijumaa ya mji wa Subeika nchini Bahrain aliatoa madai ya uongo ya kupewa hongo Ayatullahil Udhma Ali Sistani na Wamarekani kwa lengo la kurahisisha uvamiwaji wa Iraq na pia kutoa fatuwa ya kutouliwa askari wa Marekani nchini humo. 720515