IQNA

Jumuiya ya Nchi za Kiislamu IOC yawataka Wakristo waufahamu zaidi Uislamu

12:00 - December 30, 2010
Habari ID: 2055855
Ekmelledin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC ametoa taarifa akiwatakia Wakristo wote duniani mwaka mpya wa Miladia wenye furaha huku akiwasihi wazingatie na kufanya juhudi za kufahamu zaidi mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Katika taarifa hiyo Ihsanoglu amewapongeza Wakristo wote duniani wakiwemo wale wanaoishi katika nchi za Kiislamu kwa mnasaba wa kuwadia Krismasi ya kuzaliwa Nabii Isah (as) pamoja na kuingia mwaka mpya wa Milaadia.
Amesema siku ya kuzaliwa Nabii Isah ni wakati ulio na umuhimu mkubwa kwa Wakristo na kwamba ni idi ya mahaba, amani, usalama na usawa kwa wanadamu wote. Amewataka Waislamu kote duniani kushirikiana na ndugu zao Wakristo katika kusherehekea siku hii muhimu ya kimaanawi na yenye thamani kubwa.
Pia amewataka Wakristo wanaoishi katika nchi za Kiislamu kutozihama nchi hizo.
Ekmelledin Ihsanoglu amesisitiza mwishoni mwa taarifa hiyo udharura wa kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini zote za mbinguni na kuwataka Wakristo na hasa wale wanaoishi katika nchi za Magharibi kufanya juhudi za kutalii na kufahamu vyema mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. 720980
captcha