IQNA

Mfumo wa kukagua benki za Kiislamu Zambia waanzishwa

12:15 - January 01, 2011
Habari ID: 2056230
Benki Kuu ya Zambia imeanzisha mfumo unaohitajika kukagua na kuratibu shughuli huduma benki za Kiislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Lusaka, Caleb Fundanga Gavana wa Benki Kuu ya Zambia amesema wafanyakazi wa benki hiyo wamepata mafunzo maalumu kuhusu mfumo wa benki za Kiislamu.
Fundanga amesema kuwa anasubiri sekta binafsi nchini humo itoe ombi la kuanzisha benki za Kiislamu nchini Zambia. Gavana wa Benki Kuu ya Zambia amesema benki hiyo iko tayari kupokea maombi ya kuanzishwa benki za Kiislamu nchini humo.
Fundanga ameelezea matumaini kuwa kuanzishwa benki za Kiislamu zinazotoa mikopo bila kutoza riba kwa wateja ni jambo ambalo litapugunza gharama za mikopo nchini humo.
721516
captcha