IQNA

ISESCO yataka kutolewe adhabu kali kwa waliotekeleza shambulio la Alexandria

16:43 - January 03, 2011
Habari ID: 2058241
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO limetaka kutolewe adhabu kali kwa magaidi waliotekeleza shambulio dhidi ya kanisa na al-Qiddissin katika mji wa Alexandria nchini Misri.
Taarifa ya ISESCO imelaani vikali shambulio hilo ikisema kuwa ni jinai kubwa iliyolenga wananchi wa Misri na usalama wa nchi hiyo. Imesema mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu yanalaani na kupinga vikali vitendo kama hivyo.
ISESCO imetuma rambirambi kwa familia za Wamisri waliouawa katika shambulizi hilo la kigaidi na kusisitiza juu ya udharura wa kuungana Waislamu na Wakristo kwa ajili ya kupambana na njama hizo zinazotaka kuvuruga usalama.
Gari lililokuwa limetengwa mabumo lililipuka juzi Jumamosi mbele ya kanisa la al-Qiddissin mjini Alexandria na kuua watu wasiopungua 22. 723196



captcha