Hayo yamesemwa na Mshauri wa Rais wa Indonesia Zulfan Affandi wakati alipotembelea Kituo cha Uhakiki wa Kopyuta cha Nour katika mji mtakatifu wa Qum. Amesema kuwa Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia haukui kwa kasi katika maeneo ya mashariki mwa Asia hususan nchini Indonesia kutokana na uhaba wa vyanzo na kutokuwepo ulinganiaji sahihi.
Ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa vyanzo vya taaluma na elimu vya madhehebu ya Kiislamu ya Shia kwa lugha ya Kimalay ustawi wa madhehebu ya Shia nchini Indonesia unakabiliwa na mashaka mengi.
Mwakilishi huyo wa bunge la Indonesia amesema kuwa inatarajiwa kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na vyuo vikuu vya kidini vya Qum vitatafuta suluhisho la tatizo hilo kubwa.
Mshauri wa Rais wa Indonesia amesema Iran imekuwa fahari kubwa ya ulimwengu wa Kiislamu na mji mtakatifu wa Qum umekuwa mstari wa mbele katika harakati ya Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu. Amesisitiza kuwa katika kipindi cha sasa dunia ina kiu cha maarifa ya Ahlul Bait wa Mtume (saw) na harakati ya Imam Khomeini. 723317