IQNA

Wageni wafika Ghaza wakiwa na picha za Imam Khomeini na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

13:13 - January 04, 2011
Habari ID: 2058376
Msafara wa misaada ya kibinadamu wa Asia 1 umewasili katika Ukanda wa Ghaza kuvunja mzingiro wa eneo hilo huku baadhi ya walio katika msafara huo wakiwa wamebeba picha za Imam Khomeini (MA) mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei wakati wakikaribishwa na Wapalestina.
Kwa mujibu wa tovuti la televisheni ya Al Alam, wanaharakati katika msafara huo wamelaani vikali hatua ya serikali ya Misri kuwazuia Wairani na Wajordan kuingia katika Ukanda wa Ghaza. Aidha wamelaani hatua ya utawala wa Kizayuni kuzuia meli ya misaada katika maji ya kimataifa.
Misaada ya msafara huo ambayo ina uzito wa zaidi ya tani 100 za bidhaa za kitiba, kiafya, maziwa ya watoto wadogo na vifaa vinavyotumiwa na watu wenye ulemavu uliotokana na mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa eneo hilo inatazamiwa pia kuwasili katika eneo la Ghaza.
Msafara huo unajumuisha wanaharakati zaidi ya mia moja wa nchi mbalimbali za Asia na watetezi wa haki za binadamu kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Msafara huo umepokewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Serikali ya Kuvunja Mzingiro wa Gaza Ahmad Yusuf, shakhsia na viongizi wengine wa eneo hilo.
Eneo la Ukanda wa Ghaza liko chini ya mzingiro wa nchi kavu, angani na baharini uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel tokea mwaka 2007 baada ya serikali ya Hamas kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia.
Serikali ya Misri inashirikiana na utawala wa Kizayuni katika kushadidisha mzingiro huo kutokana na kufunga mpaka wake wa kuingilia eneo la Rafah ambayo ndiyo njia pekee ya kuingilia Ghaza bila ya kukabiliwa na vizuizi vya utawala wa Kizayuni.
723713
captcha