Kogamano hilo ambao ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waislamu wa Ufaransa limeandaliwa na Muungano wa Jumuiya za Kiislamu za Ufaransa UOIF kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.
Kuandaliwa vikao kadhaa, mijadala kuhusiana na hali ya kijamii na kisiasa ya Uislamu katika zama hizi, tafsiri ya Qur'ani na vyanzo vya Kiislamu na kuchunguzwa hali ya Waislamu wa Ufaransa ni miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo.
Mbali na Waislamu wa Ufaransa, shakhsia wa Kiislamu kutoka nchi nyingine za Ulaya pia hushiriki katika kikao hicho cha kila mwaka.
Japokuwa hakuna takwimu za kuaminika kuhusiana na idadi rasmi ya Waislamu wa Ufaransa lakini katika miaka ya hivi karibuni duru rasmi za serikali pamoja na vyombo vya habari vya Ufaransa vimekuwa vikisema kuwa idadi ya Waislamu wa nchi hiyo inafikia watu milioni tano. 723270