IQNA

8:57 - January 05, 2011
Habari ID: 2059166
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as):

Hakuna nguvu yoyote inayoweza kukabiliana na Uislamu duniani

Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as) Hujjatul Islam Walmuslimin Akhtari amesema kuwa hakuna nguvu yoyote duniani inayoweza kukabiliana na Uislamu au kuifuta dini hiyo na Ahlubaiti wa Mtume (saw), kwani Uislamu umo katika fitra na maumbile ya wanadamu.

Tovuti ya Shiite News imeripoti kuwa, Hujjatul Islamu Walmuslimin Akhtari ameyasema hayo katika mazungumzo yake ya ujumbe wa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Jamhuri ya Azerbaijan. Ameongeza kuwa atamuandikia barua Rais Ilham Aliyev wa nchi hiyo katika juhudi za kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo.
Katika mazungumzo hayo, kiongozi wa zamani wa Waislamu wa Azerbaijan Ali Ikram Aliyev alitoa ripoti fupi kuhusu hali ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo na mapambano yao ya kishujaa ya kukabiliana na marufuku ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu katika vyuo vikuu.
Ujumbe wa Mashia wa Azerbaijan pia umekosoa hatua ya serikali ya nchi hiyo na kusema imepiga marufuku vazi la hijabu katika vyuo vikuu bila ya kuidhinishwa na bunge. Umesisitiza kuwa Waislamu wa madhehebu ya Shia wa Azerbaijan hawatafumbia macho itikadi zao na watapambana kwa nguvu zao zote na hujuma zinazofanywa dhidi ya dini na propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu Uislamu. 724401


captcha