IQNA

Baraza la Wanazuoni wa Kishia la Bahrain launga mkono kiongozi wa Mashia wa nchi hiyo

11:42 - January 06, 2011
Habari ID: 2059837
Baraza la Wanazuoni wa Kishia wa Bahrain limetoa taarifa likilaani vikali hujuma inayofanywa na baadhi ya watu dhidi ya Ayatullah Sheikh Isah Ahmad Qassim, kiongozi wa Mashia wa Bahrain na kuwataka wananchi wa nchi hiyo waunge mkono na kumtetea kiongozi huyo.
Tarifa hiyo imesema kuwa katika uhai wake wa kisiasa na kijamii, Bahrain imekuwa na shakhisa na viongozi wengi lakini hadi sasa haijawahi kuwa na shakhia kama Ayatullah Sheikh Isah Qassim ambaye ana sifa zote njema anazopasa kuwa nazo kiongozi wa kidini kama imani, kiwango cha juu cha elimu, muono mpana, ushujaa na hekima, zuhudi na ikhlasi, subira na uvumilivu, kukubalika na umma na mwenye maneno yanayopenya kwenye nyoyo za watu.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kuwepo Sheikh Isah nchini Bahrain ni neema kubwa kwa nchi hiyo, ambapo maneneo na misimamo yake haipendelei upande wala kundi lolote na kwamba anazingatia kwa umakini mkubwa maslahi ya taifa la nchi hiyo.
Imesema Mashia wa Bahrain wanamtii Ayatullah Sheikh Isah Qassim kutokana na maamrisho ya kidini ya kutii marja' na kiongozi aliyetimiza masharti ya kuwa kiongozi wa Waislamu, ambapo masharti hayo yamekusanyika kwenye shakhsia huyo.
Taarifa ya baraza lililotajwa la Mashia wa Bahrain imesisitiza kuwa Wabahrain wataendelea kumfuata kiongozi huyo aliyetimiza masharti ya uongozi na kwamba hawatababaishwa na fitina za wafitini. 724856
captcha