IQNA

Toleo jipya la “Mkakati wa Kuyakurubisha Madhahib ya Kiislamu”

11:48 - January 09, 2011
Habari ID: 2060769
Shirika la Kiislamu la la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO limechapisha toleo jipya la jarida la, ““Mkakati wa Kuyakurubisha Madhahib ya Kiislamu” kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kifaransa. Mkakati huu wa ISESCO uliidhinishwa katika Kikao cha Kumi cha Viongozi wa Kiislamu kilichofanyika nchini Malaysia mwaka 2003.
Dr. Abdulazizi Othman Altwaijri, Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO ameandika utangulizi wa jarida hilo.
Katika utangulizi wake, Dr. Altwaijri amesema mkakati huu uko katika msingi wa mitazamo ya pamoja ambayo inaunganisha badala ya kutenganisha, unaleta pamoja badala ya kutenganisha na inaimarisha badala ya kuudhoofisha umma wa Kiislamu.
Amesema juhudi za mkakati huo zinakusuduia kuleta mshikamano wa Kiislamu na kuimarisha ile hisia ya Waislamu kuwa katika umma mmoja wa Kiislamu kwa mujibu wa maneneo ya Mwenyezi Mungu anaposema: “Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungelitoa vyote viliomo duniani usingeliweza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima”. Surat Al- Anfaal 63
726085
captcha