Kwa mujibu wa tovuti ya Palestina Info, madaktari hao ambao walikuwa wakizungumza na waandishi habari baada ya kuyatembelea maeneo ya mashambulio hayo ili kutathmini hali ya afya ya eneo hilo wamesema kuwa Gaza imejaa watoto waliolemazwa na silaha hizo zilizopigwa marufuku zikiwemo za fosfori, urani uliyohafifishwa, mabomu ya vishada na silaha nyingine nyingi za kemikali.
Madaktari hao pia wametaka kuondolewa mara moja kwa mzingiro unaotekelezwa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ili kuwezeshwa kufikishwa misaada ya dharura kwa watoto na watu wengine wanaohitajia misaada ya kibinadamu na hasa ya kiafya na kitiba katika ukanda huo.
Askari wa Israel wanazuia kuingizwa katika ukanda huo shehena za kitiba na pia kuondoka wagonjwa wa ukanda huo ili kutibiwa katika nchi nyingine. Kutokana na mzingiro huo wagonjwa wengi wa ukanda huo wamekuwa wakipoteza maisha yao. 727189