Kwa mujibu wa tovuti ya Palestine info, Martin Nesirky, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kwamba Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa umoja huo amelaani uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kubomoa nyumba hiyo iliyoko katika eneo la Sheikh Jarrah, Quds Mashariki na ambayo sasa imebadilishwa na kuwa hoteli kwa jina la Shepherd. Amesema hatua hiyo bila shaka itazua mvutano katika eneo hilo.
Nesirky amesema, utawala wa Israel hauupi umuhimu wowote wasiwasi wa jamii ya kimataifa kuhusiana na ukiukaji wa sheria ya kutojengwa majengo mapya ya utawala huo katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu.
Sheikh Raid Swalah, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina amelaani vikali hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni na kusisitiza kwamba ndoto ya utawala huo ya kuyahudisha Quds na kujenga hekalu la ngano juu ya Quds iliyoharibiwa kamwe haitathibiti.
Muhammad al-Agha Waziri wa Utalii wa Palestina pia amelaani uamuzi huo na kusema kuwa unatekelezwa katika fremu ya siasa za utawala huo za kuharibu maeneo ya Kiislamu na kuwafukuza Wapalestina katika ardhi zao huko Quds Tukufu. 728689