Akizungumza hivi karibuni mbele ya waandishi habari, Haj Salim Musa, mmoja wa viongozi wa jamii ya Kiislamu ya Albania amebainisha wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na uwezekano wa kupasishwa mswaada huo bungeni.
Haj Musa ambaye hivi karibuni anapanga kukutana na Waziri wa Elimu wa Albania kujadili asuala hilo amesema kuwa hijabu si nembo ya kawaida bali ni jambo linalofaradhishwa na dini kwa mabinti na wanawake wote wa Kiislamu. Amesema marufuku dhidi ya vazi hilo katika sekta ya kitaifa ya elimu ni upuuzaji wa wazi wa haki ya masomo na maisha ya kijamii kwa Waislamu ambao wanaunda sehemu kubwa ya jamii ya Albania.
Sehemu kubwa ya jamii ya Albania inaundwa na Waislamu kisha Waorthodox na Wakatoliki. 729284