IQNA

Pakistan yawataka Waislamu kukumbatia sayansi na teknolojia

12:08 - January 13, 2011
Habari ID: 2063877
Waziri Mkuu wa Pakistan Sayid Yusuf Raza Gilani amewataka Waislamu duniani kuungana katika kuanzisha miradi ya sayansi na teknolojia ili kukabiliana na changamoto za karne ya 21.
Gilani amesema wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC wanapaswa kuwekeza zaidi katika sayansi na teknolojia ili kwenda sambamba na maeneo mengine duniani.
Gilani alikuwa akuhutubia kikao cha 14 cha Kamati ya OIC ya Sayansi na Ushirikiano ya Kitekonolojia COMSTECH kilichoandaliwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia mjini Islamabad.
Kikao hicho cha siku mbili kilichoanza Jumanne 11 Januari kilijadili miradi ya sayansi na miradi mikubwa ya kukutanisha pamoja uwezo wa nchi za Kiislamu. “Tunaishi katika zama za ubunifu wa kisayansi na ustawi wa teknolojia. Katika jamii zilizojengwa chini ya msingi wa elimu katika karne ya 21, mataifa yatakayofanikiwa ni yale yatakayotia fora katika sayansi na teknolojia”, amesema Waziri Mkuu wa Pakistani.
Gilani ameashiria mchango mkubwa wa wasomi Waislamu waliokuwa waanzilishi wa sekta ya sayansi na tiba katika kipindi cha miaka 600. Amesikitika kuwa zama bora za kunawiri kisayansi umma wa Kiislamu zilifika ukingoni kutokana na ukosefu wa uongozi wa kielimu.
Gilani amesema kuwa Iran, Saudi Arabia, Syria na Pakistan zimetoa mchango wa dola milioni tano kila moja katika bajeti ya US$ milioni sabini kwa ajili ya miradi ya sayansi na teknolojia ya Kamati ya OIC ya Sayansi na Ushirikiano ya Kiteknolojia.
729501
captcha