Kwa swala hiyo Waislamu wamedhihirisha malalamiko yao dhidi ya hatua hiyo iliyochukuliwa na wasimamizi wa mji wa New Delhi.
Waislamu hao wapatao 1500 waliswali swala hiyo ya Ijumaa chini ya usimamizi mkali wa askari usalama 2000.
Siku ya Jumatano asubuhi, Shirika la Ustawi wa New Delhi lilibomoa msikiti uliotajwa kwa kisingizio kuwa ulikuwa umejengwa kwenye uwanja wa umma jambo lililozusha malalamiko na maandamano makubwa ya Waislamu wa mji huo.
Sehemu kubwa ya mji wa New Delhi ilifungwa kwa masaa kadhaa kufuatia maandamano ya malalamiko yaliyofanywa na Waislamu mara tu baada ya swala ya Ijumaa. 730623