Kwa mujibu wa Idara ya Mahusiano ya Umma ya Jumuiya ya Ahlul Beit (as) mkutano huo ulioandaliwa kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamno kati ya Mashia na Masuni ulifanyika siku za Ijumaa na Jumamosi za tarehe 14 na 15 Januari.
Sofia Bek Latif mmoja wa waandaaji wa mkutano huo amesema kuwa uliandaliwa kwa madhumuni ya kuondoa vizuizi vinavyozuia kupatikana umoja wa Kiislamu. Viongozi wa Kiislamu wakiwemo wa Kishia na Kisuni kutoka kote Marekani na Waislamu wenye asili ya Kiarabu, Kiasia na Kiafrika wamehudhuria mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Jumuiya za Kiislamu za Michigan na Jumuiya za Kiislamu za Marekani Kaskazini ISNA.
Ni vyema kukumbusha hapa kwamba mwaka 2006 pia viongozi wa Kishia na Kisuni wa Detroit walitia saini hati ya maelewano ya kuwazuia Waislamu kutuhumiana na kutumia katika maandishi yao maneno yanayowakaribisha pamoja zaidi Waislamu na si ya kuwatenganisha. 731285