Gazeti la al Yaoum al Saab'i linalochapishwa Misri limeripoti kuwa al Darini amesema askari usalama wa nchi hiyo wanafuatilia kwa makini harakati za Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mikoa 17 ya Misri na wanawatia nguvuni wafuasi wa madhehebu hiyo bila ya sababu yoyote.
Katibu wa Baraza Kuu la Ahlulbait (as) la Misri ameashiria matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Sheikh Mkuu wa al Azhar Ahmad al Tayyib aliyetaka kukomeshwa vitendo vya kuwakandamiza Mashia nchini humo na akasema: "Hii leo Waislamu wa madhehebu ya Shia wanaswekwa jela bila ya kufanya kosa lolote na tunaitaka serikali ya Misri kukomesha mwenendo huo."
Amesema viongozi wa Misri wanapaswa kuelewa kwamba wakazi wengi wa eneo la Sinai ni wafuasi wa madhehebu ya Shia na kwamba wafuasi wa madhehebu nyingine wanaoishi katika eneo hilo wana mitazamo inayokaribiana mno na ya Shia. 732002