IQNA

Moscow, mwenyeji wa kongamano la kwanza la Waislamu wa Ulaya

12:58 - January 20, 2011
Habari ID: 2067821
Kongamano la kwanza la Waislamu wa Ulaya limepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Russia Moscow mwezi Juni ujao.
Akizungumzia suala hilo siku ya Jumapili, Ravil Gainutdin, Mkuu wa Baraza la Mamufti wa Russia amesema kuwa kongamano hilo litafanyika kutokana na maombi mengi ambayo yametolewa na Waislamu wa nchi tofauti za Ulaya. Amesema pendekezo la kufanyika kongamano hilo nchini Russia pia limekaribishwa na Ekemeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC ambaye amesema kuwa yuko tayari kushiriki kwenye kongamano hilo.
Ravil Gainutdin amesema kuwa kongamano hilo ni hatua muhimu katika njia ya kuimarisha amani, urafiki na maelewano kati ya Waislamu kwa msingi wa thamani za Kiislamu. Amezitaka taasisi za kidini, wanasiasa na wanafikra wa kidini kupambana na misimamo ya kupindukia mipaka na kuongeza kuwa jamii ya Waislamu wa Russia haipasi kuachwa nyuma katika kulinda amani na utulivui wa nchi hiyo. 733713
captcha