Kwa mujibu wa shirika la habari la Imarati WAM, Waziri Mahmoud al-Habash ametoa taarifa akisema kuwa kuharibiwa kwa makuburi hayo mengi ya masahaba wa Mtume (saw), wanazuoni na Waislamu wa kawaida na utawala wa Kizayuni ni ochokozi na dharau ya wazi kwa thamani za Kiislamu na Kiarabu katika mji mtakatifu wa Quds na vilevile jinai za kibaguzi ambazo bila shaka zitaamsha hasira ya Waislamu kote ulimwenguni.
Waziri huyo vilevile amesisitiza juu ya udharura wa kulindwa maeneo matakatifu ya Waislamu huko Palesina na kuongeza kuwa licha ya Wapalestina, hilo ni jukumu zito linalopaswa kutekelezwa na Waislamu pamoja na watetezi wote wa haki na uhuru duniani.
Al-Habash vilevile amezitaka nchi zote za Kiarabu na Kiislamu, Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuchukua msimamo mmoja wa Kiislamu na Kiarabu kwa lengo la kupambana na jinai za Wazayuni ili kulinda matukufu ya Waislamu na Wakristo huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala dhalimu wa Israel. 734258