Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kiku cha al Azhar cha Misri imefuta uteuzi wa mgombe wa zawadi ya kimataifa ya utafiti wa Kiislamu ya Zainul Abid bin Ali, rais aliyeng’olewa madarakani wa Tunisia.
Taarifa ya Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya Chuo Kiku cha al Azhar imesema jumuia hiyo haitapendekeza jina na mwanachama wake, mwanazuoni au msomi yeyote wa Misri kwa ajili ya zawadi ya rais aliyeng’olewa madarakani wa Tunisia ambayo ina thamani ya dinari elfu 30.
Kikao cha Jumuiya hiyo pia kimechunguza tena mpango wa kuzidisha adhabu ya kuchapisha nakala zenye makosa za Qur’ani Tukufu na Hadithi za Mtume (saw). Kwa mujibu wa mpango huo, taasisi au mtu yeyote atakayochapisha Qur’ani au Hadithi za Mtume zenye makosa ya kichapa atafungwa jela miaka 15, kupigwa faini ya lira elfu tano za Misri na kusimamishwa kazi kwa kipindi cha miaka mitatu. 737580