IQNA

Uwezo wa Saudi Arabia wa kupokea mahujaji kuongezeka hadi mahujaji milioni 10

16:59 - January 30, 2011
Habari ID: 2072629
Meya wa mji mtakatifu wa Makka ametangaza kuwa kufikia miaka mitatu ijayo Saudi Arabia itakuwa na uwezo wa kupokea mahujai milioni 10.
Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Gazette, Meya Usama bin Fadhil al-Bar amesema kuwa dola bilioni 27 zimetengwa kwa ajili ya kupanua na kuubadilisha mji wa Makka kuwa mji wa kisasa katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Ameongeza kuwa kuongezwa uwezo wa Saudia wa kuwapokea mahujaji ni miongoni mwa mipango ya mradi huo mkubwa wa ustawi. 738332
captcha