IQNA

Mustakbali wa uhusiano wa Uislamu na Magharibi kuchunguzwa Montana, Marekani

12:37 - February 01, 2011
Habari ID: 2073872
Mustakabali wa uhusiano wa Uislamu na nchi za Magharibi unatazamiwa kuchunguzwa katika kikao kilichopangwa kufanyika tarehe 16 Februari katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Montana nchini Marekani.
Kwa mujibu wa tovuti ya chuo hicho Mtontana.edu, John L. Esposito, profesa wa masuala ya Kiislamu na kimataifa wa mjini New York anatazamiwa kuzungumza katika kikao hicho ambacho kitaanza saa moja usiku kwa wakati wa jimbo hilo. Mwanafikra huyo wa Kiislamu atazungumzia fikra potofu na tuhuma zinazotolewa na Wamagharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Esposito ni muhadhiri wa masuala ya Kiislamu na kimataifa katika Chuo Kikuu cha Georgetown. Kufikia sasa ameandika vitabu na makala 35 yanayohusiana na Uislamu na kitabu chake cha hivi karibuni ni kile kinachohusiana na mustakbali wa Uislamu kilichochapishwa mwaka uliopita wa 2010. 740257
captcha