Suala la uwezekano wa kutolewa mafunzo ya Kiislamu katika shule za Uswisi limechunguzwa katika kipindi maalumu cha televisheni ya nchi hiyo ambapo Amina Shakir, mkuu wa mafunzo ya vyuo vikuu kwa walimu wa masomo ya kidini nchini humo ameshiriki.
Shakir ambaye alikuwa mgeni maalumu wa kipindi cha Sternstunde Religion katika televisheni ya Uswisi ya Schweizer TV amechambua kwa kina uwezekano wa kutolewa masomo hayo ya Kiislamu katika shule za Uswisi.
Japokuwa suala hilo limekuwa likipingwa vikali na mirengo ya wanasiasa wa nchi hiyo lakini limekuwa likijadiliwa kwa kina na wataalamu wa masomo nchini.
Tunaashiria hapa kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopitishwa nchini Uswisi mwaka 1912 wanafunzi wa Kiislamu wana haki sawa na wenzao wa Kikristo kwa ajili ya kujifunza masomo ya dini yao tukufu ya Kiislamu. Kwa msingi huo nchi hiyo imekuwa ikitoa vipindi maalumu vya masomo kwa viwango vya chuo kikuu kwa walimu walio na hamu ya kufundisha masomo ya Kiislamu katika shule za nchi hiyo. 744007