IQNA

Mwanafikra wa Kishia wa Misri apongeza uungaji mkono wa Hizbulllah kwa Wamisri

12:21 - February 10, 2011
Habari ID: 2078708
Ahmad Rasim an-Nafis mwanafikra wa Kishia wa Misri amepongeza na kutoa shukrani kwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah kutokana na uungaji mkono wake kwa harakati za mapinduzi za wananchi wa Misri dhidi ya utawala wa kidikteta wa Rais Hosni Mubarak nchi hiyo.
Amesema uungaji mkono huo umetimia katika mkondo wa uungaji mkono wa kishujaa wa Ayatullahil Udhma Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa mapinduzi hayo ya Misri. Amesema, uungaji mkono wa shakhsia wawili hao wa Kiislamu una umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Misri wanaopigania demokrasia na uongozi bora nchini kwao. An-Nafis amesema historia ya Misri inathibitisha wazi kwamba utawala wa Mubarak daima umekuwa ukihudumia Marekani na utawala haramu wa Israel katika Mashariki ya Kati na kwamba kwa kueneza propaganda sumu na zisizo na ukweli wowote kwamba Iran inataka kujipanua na kueneza Ushia na wakati huohuo kuzusha hofu na kuwakandamiza wananchi wa Misri, serikali dhalimu ya Mubarak imekuwa ikihudumia kwa kila njia siasa za Tel Avi na Washington kwa madhara ya umma wa Kiislamu.
Amesema serikali hiyo imekuwa ikieneza sumu na uadui miongoni mwa Waislamu kwa kueneza siasa za chuki za kimadhehebu nchini Misri na katika nchi nyingine za Kiarabu. Amesema baadhi ya mirengo ya kisiasa nchini humo inashirikiana na Wazayuni na Wamarekani katika kuzuia Misri kurejea katika nafasi yake halisi katika ulimwengu wa Kiislamu na Kiarabu kwa sababu jambo hilo bila shaka litadhuhuru na kuhatarisha maslahi yao katika eneo.
Mwanafikra huyo wa Kiislamu amekosa vikali siasa za Saudi Arabia ambayo inashirikiana kwa karibu na mirengo ya kimadhehebu nchini Misri na vilevile Marekani pamoja na Wazayuni kwa shabaha ya kumbakisha madarakani Dikteta Mubarak.
Mwanafikra huyo wa Misri amesema mwishoni kwamba Marekani inadai kuwa inataka marekebisho ya kidemokrasia yatimie nchini Misri ilihali inajaribu kila iwezalo kumbakisha Dikteta Mubarak katika nafasi yake ili aendelee kudhamini maslahi haramu ya Wamagharibi nchini humo. 745314
captcha