IQNA

Gazeti la ‘Muslim News’ laanzishwa Ghana

11:30 - February 19, 2011
Habari ID: 2082821
Kwa mnasaba wa mwaka wa 32 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, gazeti la kila siku la ‘Muslim News’ limeanzishwa Ghana.
Jumuiya ya Waislamu Ghana ikishirikiana na Idara ya Utamaduni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Accra imeanzisha gazeti hilo la kwanza la Waislamu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Toleo jipya la jarida hilo lina maudhui kama vile ‘Maadili kwa Mtazamo wa Imam Khomeini’ na vile vile matukio muhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Waislamu nchini Ghana wamekaribisha gazeti hilo ambalo wanasema litakuwa la kwanza na la aina yake kuakisi hali na mitazamo ya Waislamu nchini humo.
749030
captcha