IQNA

Mkutano wa tatu wa kimataifa wa uchumi wa Kiislamu kufanyika Russia

14:07 - February 20, 2011
Habari ID: 2083506
Mkutano wa tatu wa kimataifa wa uchumi wa Kiislamu na uwekezaji umepangwa kufanyika tarehe 13 na 14 Mei mwaka huu katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
Tovuti ya Islamicbanking.ru imeripoti kuwa mkutano huo utafanyika kutokana na kupanuka ustawi wa uchumi wa Kiislamu nchini Russia na kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wadau na wataalamu wa masuala ya uchumi na uwekezaji wa Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali duniani kwa shabaha ya kuchunguza masuala ya uchumi wa Kiislamu.
Wawakilishi wa sekta za masoko, wataalamu na washauri wa masuala ya uchumi wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali watachunguza maendeleo ya sekta ya fedha na ya Kiislamu na vilevile fursa mpya za kuvutia vitega uchumi katika sekta hiyo.
Masuala mengine yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na mbinu, nyenzo na sheria za ustawi wa uchumi wa Kiislamu nchini Russia. 750364

captcha