Moja ya makosa ambayo hayawezi kusameheka ya kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi ni kutoa dharba dhidi ya Sayyid Mussa Sadr na hii ni dhambi kubwa zaidi ya jahili huyu, kwani jamii ya Kiislamu ya Lebanon imempoteza mwanafikra hodari aliyehimiza umoja na mshikamano.
Hayo yamesemwa na Sayyid Yahya Yathribi, mhadhiri mstaafu na mwandishi wa tafsiri ya Qur'ani ya Ruz. Ameongeza kuwa Imam Mussa Sadr ni miongoni mwa wasomi wachache wa zama hizi na shakhsia wa kipekee ambaye angesaidia sana juhudi za kuwaunganisha Waislamu na wanadamu wengine lakini Muammar Gaddafi amekwamisha harakati za msomi huyo wa Kiislamu kwa kipindi cha miaka 32.
Mwandishi huyo wa kitabu cha Irfani ya Kimatendo katika Uislamu amezungumzia jinsi mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu alivyotekwa nyara na kufungwa na Kiongozi wa Libya Gaddafi kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na akasema baada ya harakati kubwa za kuwaunganisha Waislamu, jiuhudi za kuwatetea wananchi wa Palestina na hata kutetea wafungwa wa kisiasa, Imam Mussa Sadr alikwenda Libya kwa mwaliko wa Kanali Muammar Gaddafi na akatekwa nyara huko huko na utawala wa nchi hiyo.
Amesema wakati huo Gaddafi alikana kuhusika na kutoweka Sayyid Mussa Sadr na kudai kuwa ameelekea Roma, Italia lakini uchunguzi umethibitisha kuwa msomi huyo wa Kiislamu hakuondoka katika ardhi ya Libya. 755308