Taarifa hiyo imesema kwamba dikteta Muammar Gaddafi amewasha moto ambao utamchoma yeye mwenyewe. Imeendelea kusema kwamba Gaddafi amewapoteza marafiki na washirika wake wa karibu zaidi katika matukio ya hivi karibuni na kulaani kitendo chake cha kuwatumia mamluki wa kigeni katika kuwakandamiza wananchi ambao wanafanya maandamano ya amani kupinga dhulma na uonevu wa utawala wake.
Jumuiya hiyo imesisitiza kwamba Gaddafi hataepuka adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo amemuainishia kutokana na dhulma aliyowafanyia Walibya.
Taarifa ya jumuiya hiyo ya wanafikra wa Kiislamu imesisitiza kwamba hivi sasa Walibya wameamua kuhuisha historia yao yenye fahari na kwamba katika kufikia lengo hilo Mummar Gaddafi hatakuwa na njia nyingine ya kukwepa ghadhabu yao isipokuwa kukabiliwa na hatima kama ile iliyowapata hivi karibuni madikteta wa Tunisia na Misri. 756893