IQNA

Takwa la mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mkoani Qatif, Saudia

18:11 - March 06, 2011
Habari ID: 2091227
Hujjatul Islam wal Muslimeen Abdul Karim al-Jalil mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Saudi Arabia ambaye pia ni mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei mkoani Qatif amewataka watawala wa Saudi Arabia wamwachilie huru mara moja Sheikh Taufiq al-Aamir, hatibu wa Kishia wa swala ya Ijumaa ya mji wa Ihsaa.
Kwa mujibu wa kanali ya habari ya Rasid, Sheikh al-Jalil hatibu wa swala ya Ijumaa ya mji wa ar-Rubeiiyya katika mkoa wa Qatif amewataka watawala wa Saudi Arabia wamwachilie huru haraka iwezekanavyo mwanazuoni huyo ambaye walimtia mbaroni kwa hoja ya kutaka kuasisiwa nchini humo ufalme wa kikatiba na kuondolewa mfumo wa ubaguzi wa kimadhehebu. Amesema takwa hilo la al-Aamir ni takwa dogo sana kati ya matakwa mengi ambayo mataifa yaliyoendelea yanayafuatilia. Tokea kutiwa nguvuni Sheikh Taufiq al-Aamir, zaidi ya wanazuoni mashuhuri 100 wa Kishia katika miji ya Ihsaa na Qatif wametoa taarifa tofauti wakitaka kuachiliwa mara moja kwa hatibu huyo wa Kishia na pia wafungwa wengine ambao wametiwa mbaroni kwa kutokana na maoni na itikadi zao.
Siku ya Ijumaa wakazi wa Ihsaa pia walifanya maandamano ya amani wakitaka kuachiliwa huru kwa Sheikh Taufiq al-Aamir. 758561
captcha