Hatua za utawala haramu wa Israel za kuyahudisha mji mtakatifu wa Quds zitachunguzwa hivi karibuni huko Amman mji mkuu wa Jordan na kamati ya wataalamu wa mambo ya kale ya Shirika la Elimu, Sayansi na utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Kikao hicho kimepangwa kufanyika tarehe 16 na 17 za mwezi huu wa Machi. Kikao hicho ambacho kinafanyika kwa ushirikiano wa Shirika la Mambo ya Kale la Jordan kitachunguza na kujadili hatua za kichokozi na za kichochezi za Wazayuni za kuongeza Misiki ya Ibrahim huko al-Khalil na Bilal bin Rabah ulioko Beit al-Laham katika orodha ya turathi za Mayahudi.
Kikao hicho pia kitayalalamikia mashirika ya kimataifa yanayohusika na masuala ya turathi na mambo ya kale kuhusu hatua hizo za kichokozi za Wazayuni katika maeneo ya Waislamu. 762042