IQNA

Uungaji mkono wa Muungano wa Kimataifa wa Maulama kwa Mapinduzi ya Yemen

14:11 - March 14, 2011
Habari ID: 2095475
Muungano wa Kimataifa wa Maulama wa Kiislamu umetoa taarifa ukiunga mkono matakwa halali na mapinduzi ya wananchi wa Yemen.
Katika taarifa hiyo muungano huo umesema kuwa unafuatilia kwa wasiwasi mkubwa matukio ya hivi sasa ya Yemen na maandamano ya amani ya watu wa nchi hiyo katika kupambana na ufisadi, dhulma, uonevu pamoja na hujuma ya kinyama inayotekelezwa dhidi yao na utawala wa nchi hiyo. Taarifa hiyo imeashiria hujuma kali inayotekelezwa na askari jeshi wa Yemen dhidi ya wananchi na kupelekea mamia kati yao kuuawa na kujeruhiwa na kusisitiza kwamba jambo hilo linafanyika kinyume cha sheria kwa ajili ya kuubakisha madarakani utawala wa Rais Ali Abdallah Swaleh. Imesema maandamano ya amani ni haki ya wananchi wa Yemen na kwamba yanafanyika kwa lengo la kutaka mabadiliko yafanyike katika mfumo wa utawala wa nchi hiyo jambo ambalo imesema linashajiishwa na thamani za Kiislamu. 762742
captcha