Kwa mujibu wa tovuti ya OIC Ihsanoglu amesema kuwa Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu wana wasiwasi mkubwa kuhusiana na maafa yaliyowapata wanadamu wenzao huko Japan na kuongeza kuwa jumuiya ya OIC pamoja na nchi zote wanachama ziko tayari kuwasaidia wananchi wa nchi hiyo kwa msaaada wowote ule wanaoweza kutoa.
Amesema anatumai hali ya nchi hiyo itarejea katika hali ya kawaida hivi karibuni. 763247