Haya ni kwa mujibu wa Adel Awn mwakilishi wa Harakati ya Amal mjini Tehran alipozungumza katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu 'Nafasi ya Imam Musa Sadr katika Mwamko wa Kiislamu Duniani' lililofanyika Machi 12 mjini Tehran.
Amemtaja Imam Musa Sadr kuwa kiongozi wa kipekee kwa maneno na vitendo. "Alikuwa mwanazuoni wa kipekee katika masuala ya umaanawi, siasa na jamii", amesema.
"Imam Musa Sadr alisisitiza umuhimu wa mazungumzo baina ya tamaduni na kujenga misingi ya kuaminiana. Aliweza kutamabua vyema njama za maadui. Alianzisha harakati ya mapambano ya Lebanon kwa lengo la kulinda ardhi ya kusini mwa nchi hiyo na Ardhi Takatifu za Palestina", ameongeza.
Awn ameashiria kutoweka Imam Musa Sadr na kusema kuwa alitekwa nyara na dikteta Gaddafi kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
Mwakilishi wa Harakati ya Amal ambayo iliasisisiwa na Imam Musa Sadr amemtaja mwanazuoni huyo aliyetoweka kuwa mwanazuoni mnyenyekevu.
Kongamano la Kwanza la Kimataifa kuhusu 'Nafasi ya Imam Musa Sadr katika Mwamko wa Kiislamu Duniani' limeandaliwa na Harakati ya Kimataifa ya Kuachiliwa Huru Imam Musa Sadr.
762642