Katika taarifa ya mwisho, washiriki wa kongamano hilo walisisitiza kuhusu utekelezwaji maamuzi ya vikao vilivyopita.
Aidha iliafikiwa kuwa kubuniwe jumuiya ya kisayansi ya wafuasi wa dini mbalimbali kwa lengo la kuandika hati ya "Sayansi na Imani".
Kuhusu umuhimu wa miujiza ya Qur'ani na Suna ya Mtume SAW, wanazuoni na wasomi walioshirikia walisisitiza umuhimu wa kuchapishwa vitabu na utafiti wa kisayansi kuhusu mada hizo na kusambazwa vitabu hivyo katika maktaba, vyuo vikuu na taasisi za Kiislamu. Aidha kumeonekana kuwepo haja ya kufasiri utafiti uliofanyika kwa lugha mbalimbali duniani.
Washiriki vilevile wametoa wito kwa wahisani, wawekezaji na taasisi za kiuchumi za nchi za Kiislamu kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya kusambazwa mafundisho ya Qur'ani na Suna kote duniani ili walimwengu wafahamu kuhusu sayansi katika mafundisho ya Uislamu.
Kongamano la 10 la kimataifa la 'Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani na Suna za Mtume SAW lilianza Machi 11 mjini Istanbul na lilitayarishwa na Taasisi ya Uturuki ya Utafiti wa Kiislamu.
763295