IQNA

Jumuiya ya Wifaq al-Watan ya Bahrain yakadhibisha madai ya kutaka msaada kutoka Iran

13:14 - March 16, 2011
Habari ID: 2096487
Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wifaq al-Watan ya Bahrain amekadhibisha madai kwamba jumuiya hiyo imetaka msaada kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Sheikh Salman amepinga kila aina ya uingiliaji wa mambo ya ndani ya nchi hiyo kutoka upande wowote ule. Amesema licha ya kuwa Bahrain ina hamu kubwa ya kuimarisha uhusiano wake na kila nchi jirani lakini haiko tayari kukubali uingiliaji wa nchi hizo katika mambo yake ya ndani. Baada ya kuthibitishwa ripoti za kuingia askari jeshi wa Saudi Arabia nchini Bahrain kwa lengo la kuzima mapambano ya wananchi dhidi ya wafalme dhalimu wa nchi hiyo, maadui wa Iran wameeneza uvumi kwamba jumuiya za Kishia za Bahrain kutoka Iran zimekuwa zikiingia nchini humo kuwasaidia ndugu zao wanaokandamizwa na askari wa nchi hiyo kwa ushirikiano wa askari wa Saudia. 764186
captcha