IQNA

Ahmadinejad asema Marekani imechochea uvamizi Bahrain kwa Maslahi ya Wazayuni

13:08 - March 17, 2011
Habari ID: 2097258
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa uvamizi wa vikosi vya kigeni nchini Bahrain na kusema hiyo ni njama iliyotekelezwa na Marekani kwa lengo la kukandamiza harakati ya wananchi.
Rais Ahmadinejad amesema hujuma ya kijeshi ni uzoefu mbaya ambao utafeli na kuongeza kuwa mataifa ya eneo yanapaswa kuilamu 'Marekani kwa hatua hiyo ya kihalifu. Marekani inataka kuunusuru utawala wa Kizayuni wa Israel na kukandamiza mwamko wa wananchi, kwa hivyo inaunga mkono baadhi ya serikali', amesema rais Ahmadinejad.
Rais wa Iran amesema mauaji ya umati yanayotekelezwa ni jinai ambayo itapelekea kung'olewa mizizi ya Marekani katika eneo. Rais Ahmadinejad amehoji ni vipi mtawala anataka kuendesha nchi kwa silaha na kuongeza kuwa serikali inapaswa kuwa ya wananchi. Amesema ukandamizaji wa waandamanaji nchini Bahrain hautazaa matunda. Amewataka watawala wa Bahrain kufanya mazungumzo na wananchi na kutekeleza matakwa wao.
Huku akisisitiza kuwa Marekani na nchi za Ulaya zinapaswa kupata ibra kutokana na kukalia kwa mabavu Iraq na Afghanistan, Rais wa Iran amezitaka nchi za Magharibi kuweka kando malengo na uchu wao wa kikoloni na kuwaacha wananchi wa eneo hili wajiamulie mustaqbali wao wenyewe. Matamshi ya Ahmadinejad yanaashiria ukweli huo, ambao ndio unaohesabiwa kuwa chanzo kikuu na sababu ya migogoro inayotokea hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati. Ukweli huo unashuhudiwa zaidi Afghanistan na Iraq, na ni wazi kwamba fikra za waliowengi duniani hazikubali madai ya Marekani ya kuleta demokrasia na haki za binadamu katika maeneo mengine duniani. Kwa hakika kuna maswali mengi yanayopaswa kujibiwa kuhusiana na himaya inayotolewa kwa watawala madikteta na watenda jinai katika Mashariki ya Kati katika kipindi chote cha historia, na kupewa watawala hao silaha zinazogharimu mabilioni ya dola. Viongozi wa Marekani wanajaribu kupuuza mwamko na harakati ya mageuzi inayojiri hivi sasa katika nchi nyingi za eneo, katika hali ambayo sababu kuu iliyosababisha harakati hiyo ni wananchi kuhisi kudhalilishwa na tawala tegemezi kwa Marekani. Ni wazi kuwa migogoro hiyo haitotatuliwa kwa kuchukuliwa hatua za uingiliaji na kupelekwa askari wa kigeni nchini Libya au Bahrain, kwani masuala hayo hayana matokeo mengine isipokuwa kuhatarisha maisha ya raia wasio na hatia.
765171

captcha