IQNA

Khatibu wa Ijumaa asisitiza kufanywa juhudi ili Iran ijitosheleze kiuchumi

15:39 - March 26, 2011
Habari ID: 2098089
Khatibu wa sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesisitiza ulazima wa viongozi na wananchi wa Iran kufanya jitihada za kujitosheleza katika nyanja mbalimbali katika mwaka huu wa 'jihadi ya kiuchumi'.
Katika hotuba ya sala ya kwanza ya Ijumaa mjini Tehran katika mwaka mpya wa Hijria Shamsia, Hujatul Islam wal Muslimin Kadhim Siddiqi sambamba na kuashiria kwamba Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameuita mwaka huu wa 1390 Hijiria Shamsia kuwa ni mwaka wa 'jihadi ya kiuchumi' amesema, kutekeleza mipango vyema kutapelekea kujitosheleza na kusimama kidete taifa la Iran kukabiliana na njama za maadui wa mfumo wa Kiislamu. Aidha amebainisha kuwa mpango wa kutoa ruzuku kwa uadilifu ni mpango adhimu kwa ajili ya kugawanya inavyotakiwa utajiri wa taifa na kwamba serikali na wananchi wa Iran wanapaswa kufanya jitihada ili mpango huo uzae matunda. Khatibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran pia ameashiria mageuzi yanayojiri hivi sasa Kaskazini mwa Afrika katika nchi kama vile za Misri na Tunisia na kusema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana taathira kubwa katika harakati hizo za mageuzi za wananchi. Ameongeza kuwa, njama za Marekani na madola ya Magharibi za kutumia vibaya harakati hizo za mageuzi za wananchi zimegonga mwamba.
766114
captcha