Nuskha hizo za Qur'ani zilipatikana zikiwa zimetupwa kwenye taka hizo hapo siku ya Jumanne. Habari zilizochapishwa na tovuti ya Arabianbusiness zinasema kuwa nuskha hizo zilikuwa za shule moja katika mkoa wa Taif. Askari wa kuamrisha mema na kukataza maovu wa Saudi Arabia tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na suala hilo na inasemekana kuwa idara ya masomo na malezi ya mkoa huo itasailiwa kuhusiana na tukio hilo la kusikitisha. 767256