IQNA

Waafghani waandamana kupinga kukosewa heshima Qur'ani Tukufu

17:51 - April 03, 2011
Habari ID: 2099910
Siku ya Jumamosi wananchi wa Afghanistan walifanya maandamano makubwa huko katika mji wa Kandahar kupinga kitendo cha kukosewa heshima Qur'ani Tukufu nchini Marekani, maandamano ambayo yalimalizika kwa umwagikaji damu.
Maandamano hayo yamefanyika siku moja tu baada ya kufanyika maandamano mengine kama hayo katika mji mwingine wa nchi hiyo, Mazar Shariff. Baadhi ya wanachama wa kundi la Taliban walipenya kwenye maandamano hayo na kujilipua pamoja na kuchoma moto magari na maduka na hivyo kupelekea watu 9 kuuawa na wengine 81 kujeruhiwa. Miji mingine ya Afghanistan ikiwemo ya Harat na Kabul, mji mkuu, imeshuhudia maandamano kama hayo ya kulaani kitendo hicho cha dharau cha kasisi Terry Jones wa Florida dhidi ya Qur'ani Tukufu. 767840
captcha