Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Kuwait KUNA, Tariq Shadid mkuu wa mpango huo uliopewa jina la Uhuru kwa ajili ya Palestina' amesema kuwa wanaharakati na wanachama wa mpango huo wanakusanya saini kutoka kwa raia wa nchi 27 za Ulaya zilizotia saini mkataba wa kususia bidhaa zinazozatengenezwa na Wazayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na walowezi wa Kizayuni, ili kufanikisha mpango huo. Lengo la mpango huo ambao unawashirikisha shakhsia mashuhuri wa Bunge la Ulaya ni kususia kabisa bidhaa za utawala wa Kizayuni zinazozalishwa katika vitongoji vya Wazayuni vilivyojengwa kinyume cha sheria za kimataifa katika ardhi za Wapalestina. 769254