Akilaani kitendo hicho cha dharau, Ban amesema kuwa hakuna dini yoyote duniani inayoruhusu kukosewa heshima matukufu ya dini nyinginezo. Katibu mkuu huyo alilaani kitendo hicho alipoonana na kuzungumza na wawakilishi wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu katika Umoja wa Mataifa ambao ni mabalozi wa Misri, Morocco, Pakistan, Iran na Tajikistan katika umoja huo. Baada ya mazungumzo hayo, Ban amesema kuwa kitendo hicho cha kukera cha Kasisi Terry Jones kitaamsha hasira za Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia na kusema kuwa tayari kimeshasababisha wahanga katika nchi ya Afghanistan ambapo watu 12 wamepoteza maisha yao katika maandamano ya ghasia yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni. 769720