Vyama vya wafuasi wa mrengo wa kushoto vya Ujerumani mashuhuri kwa jina la vyama vya kijani na wanademokrasia wakomonisti wa nchi hiyo wametaka kushtakiwa mahakamani Teryy Jones, kasisi wa Marekani wa jimbo la Florida aliyechoma moto Qur'ani Tukufu hivi karibuni.
Vinasema kwamba takwa lao hilo linakwenda sambamba na takwa la wabunge kadhaa wa Bunge la Ulaya waliotaka kufikishwa mahakamani kasisi huyo kutokana na kitendo chake hicho cha kukosea heshima matukufu ya Kiislamu. Vyama hivyo vinasema kuwa jela ndiyo sehemu inayomfaa kasisi huyo wa uongo kutokana na kitendo chake hicho cha kichochezi dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu na Waislamu. Viongozi wa vyama hivyo wanasema kuwa kwa kitendo chake hicho cha dharau kasisi huyo mwovu amekusudia kuchochea moto wa chuki na fitina kati ya Waislamu na Wakristo na hivyo kuanzisha vita vipya vya kidini kati ya pande mbili hizo. Tayari maandamano yamekuwa yakifanyika katika nchi kadhaa za Kiislamu na hasa Afghanistan kwa madhumuni ya kulaani kitendo hicho. 769788