IQNA

Waziri wa Ulinzi wa Iran: Waislamu ndio washindi wa mwamko wa Kiislamu

10:31 - April 07, 2011
Habari ID: 2101828
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Waislamu ndio washindi wakuu wa mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi ameongeza kuwa, Waislamu na watu watakao uhuru ulimwenguni, ndio washindi halisi wa matukio yanayoendelea kujiri katika nchi za Kiarabu na Kiislamu. Brigedia Jenerali Vahidi ameyasema hayo wakati akijibu radiamali ya matamshi ya kijuba yaliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Uingereza aliyedai kwamba, eti ulimwengu utakabiliwa na hatari ya kiusalama, iwapo matukio yanayoendelea kujiri katika eneo yataachwa yaifaidishe Iran. Waziri wa Ulinzi wa Iran ameongeza kuwa, wananchi wa eneo wamechoshwa na siasa za kikoloni, kidikteta na za uingiliaji kati za Marekani na Uingereza, na kwamba wameamua kusimama kidete kwa shabaha ya kukabiliana na ukandamizaji huo. Brigedia Jenerali Vahidi ameongeza kuwa, viongozi wa Uingereza wameingiwa na hofu na harakati hizo za Kiislamu kwa sababu wanajua wazi kwamba, harakati hizo zitapelekea kukatwa mikono ya unyonyaji na uporaji wa maliasili iliyoko katika eneo, yakiwemo mafuta na gesi unaofanywa na nchi hizo za Magharibi.
770050
captcha