Wameitaka serikali ya Riyadh iondoe askari wa nchi hiyo huko Bahrain haraka iwezekanavyo. Waandamanaji hao waliofanya maandamano hayo mara tu baada ya kumalizika swala ya Ijumaa wameitaka serikali ya Saudi Arabia pia iandae mazingira yanayofaa ya kushirikishwa kisiasa Mashia katika uaendeshaji wa nchi hiyo inayotawaliwa na ukoo wa Saud. Mbali na maandamano hayo yaliyofanyika katika mji wa Qatif maandamano mengine kama hayo yalifanyika katika mji wa al-Awamiya ambapo waandamanji walipeperusha bendera za Saudi Arabia na Bahrain pamoja na kubeba mabango yaliyowataka watawala wa Saudia waondoe mara moja askari wa nchi hiyo huko Bahrain. Waandamanaji pia wamelaani ubaguzi wa kimadhehebu unaofanywa dhidi ya Mashia na kutaka ubaguzi huo uondolewe mara moja. 770798