Wamesema kitendo cha Terry Jones cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu kimewadhuru wafuasi wa dini zote ulimwenguni. Wamesema kuwa kitendo hicho si tu kwamba kimewadhuru Waislamu wa Marekani na sehemu nyingine za dunia bali kinakinzana na thamani za kiutu na mafundisho ya Kikristo. Wametaka serikali ichukue hatua za lazima kwa ajili ya kukabiliana na vitendo kama hivyo vinavyokwenda kinyume na misingi ya kidini na kisheria nchini. Viongozi hao wa kidini wamesema kuwa wanapinga kila aina ya chuki, ubaguzi na utumiaji nguvu dhidi ya Waislamu kwa kisingizio cha uhuru wa kusema. 771140