Vijana hao wamewataka wananchi wote wa Bahrain katika wiki hii kupiga nara za 'Allahu Akbar', kusoma dua, kuwasha mishumaa na kufanya maandamano katika mitaa ya miji tofauti ya nchi hiyo ili kuadhimisha wiki hii. Taarifa hiyo imewataka Wabahrain wote washiriki kwenye mazishi ya wahanga wote waliopoteza maisha yao kutokana na mateso waliyopata kwenye jela za utawala wa ukoo wa Khalifa, familia na mawakili wa wahanga kukusanyika mbele ya ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Manama na kufanyika marasimu maalumu ya kuwakumbuka wanawake wanaoshikiliwa kwenye jela za utawala wa Bahrain. Vijana hao pia wamewataka Wabahrain kukusanyika kwenye misikiti mara tu baada ya kumalizika swala ya Ijumaa hapo tarehe 15 Aprili, na kufanya maandamano kulelekea hospitali ya as-Salmaniyya ili kuonyesha mfungamano wao na majeruhi walioko kwenye hospitali hiyo inayozingirwa na askari jeshi wa Bahrain na Saudia. 772612